Header Ads

Ufanisi wa vifaa vya kupima ubora wa afya watiliwa shaka



Je, vifaa hivi vinatoa vipimo halisi?
MICHIGAN, Marekani
UTAFITI umebaini kwamba, vifaa vingi vya kupima ubora wa afya vinatoa takwimu za kupotosha kuhusu kiwango cha kalori kinachochomwa baada ya mazoezi.

Hayo ni kulingana na uchunguzi wa vifaa hivyo katika Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani. Hata hivyo, imebainika kwamba vifaa hivyo vina uwezo wa kupima mapigo ya moyo kwa ufasaha.
Watafiti hao wamependekeza kwamba wanaoutumia vifaa hivyo wawe waangalifu hususan wanapotumia vifaa hivyo kuchagua wanachokula.
Utafiti huo umependekeza wanaotengeneza vifaa hivyo, kutoa maelezo kamili ya jinsi wanavyotoa vipimo hivyo. Vifaa vilivyofanyiwa utafiti ni Apple Watch, Fitbit Surge, Basis Peak, Microsoft Band, PulseOn na MIP Alpha 2.
Vifaa hivyo vilipatikana kuwa na makosa ya zaidi ya 20% katika kupima viwango vya nguvu ya mwili inayotumika katika mazoezi.
Daktari Euan Ashley wa chuo hicho amesema watumiaji wa vifaa hivyo wanafaa kujuzwa manufaa na upungufu wa vifaa hivyo vinavyovaliwa mikononi.

No comments

Powered by Blogger.