Ndege za Pakistan zatumiwa kusafirisha heroin hadi Uingereza

Ndege ya Shirika la Ndege la Pakistan (PIA)
KARACHI, Pakistan
SHIRIKA la
ndege la Serikali nchini, limesema kuwa linachukua hatua kuhakikisha kuwa ndege
zake hazitumiwi kubeba madawa ya kelevya baada ya dawa ya heroin, kupatikana
kwenye ndege zake mbili zinazofanya safari kuenda mjini London.
Tarehe 15
mwezi huu, maofisa wa mipaka wa Uingereza walikamata ndege iliyokuwa ikitokea
mjini Islamabad ilipowasili uwanja wa Heathrow mjini London na kuikagua kwa saa
kadhaa.
Shirika la
kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza baadaye lilisema kuwa, kiwango fulani
cha heroin kilipatikana kikiwa kimefichwa katika sehemu tofauti za ndege hiyo. Kuna
madai kuwa utawala wa Uingereza ulichukua hatua hiyo kutokana na taarifa ilizopokea
kutoka Pakistan.
Hakuna mtu
aliyekamatwa lakini rubani wa ndege hiyo hakuruhusiwa kurudi Pakistan siku
iliyofuata. Kisa hicho kilisabisha aibu kwa shirika la ndege la Pakistan,
ambalo linapata nafuu baada ya ajali mbaya iliyowaua watu wengi Desemba, mwaka
jana.
Mei 22 mwaka
huu, maofisa wa Pakistan katika uwanja wa ndege wa Islamabad, walikamata zaidi
ya kilo 20 za dawa ya heroin ndani ya ndege nyingine iliyokuwa isafiri kuenda
Heathrow.
Kwa sasa uchunguzi
unafanyika kubaini ikiwa kuna ushirikiano wa kutumiwa ndege za shirika la ndege
la Pakistan, kusafirisha madawa ya kulevya kuenda nchi za ng'ambo.
BBC
No comments