Manowari ya Marekani yapita karibu na visiwa vya China

JAKARTA,
Indonesia
MAOFISA wa
Marekani wamesema kuwa, manowari ya wanamaji wa Jeshi la Marekani imetekeleza
oparesheni maalum ya ‘uhuru wa ubaharia’ karibu na visiwa vinavyozozaniwa vya
bahari ya Kusini mwa China.
Oparesheni
hiyo karibu na kisiwa kimoja bandia kilichojengwa na China, inalenga kupinga
madai ya taifa hilo la Asia kumiliki eneo hilo. China inadai umiliki wa visiwa
na miamba ya baahari ya Kusini mwa nchi hiyo.
Mataifa
mengine pia yanadai umiliki wa visiwa hivyo pamoja na miamba. Marekani imekuwa
ikisisitiza kwamba ina uhuru wa kutekeleza oparesheni zake katika maeneo yoyote
kwenye maji ya kimataifa.
Oparesheni
hiyo imefanyika karibu na visiwa cha Spratley, ambayo China imejenga kambi ya
kijeshi, jambo ambalo limezua ghadhabu miongoni mwa mataifa jirani.
Oparesheni
hiyo ni ya kwanza tangu kuanza utawala wa Rais Donald Trump, na inalenga
kukabiliana na majaribio ya China ya kudhibiti eneo, ambalo huwa linashuhudia
shughuli nyingi za ubaharia.
Kumekuwa na
vita baridi kati ya China na Marekani, ambapo kumekuwa na lawama kuwa eneo hilo
linageuzwa kuwa la kijeshi.
Hatua hiyo
ya Marekani itaathiri pakubwa uhusiano wake na China, hususan wakati ambapo
utawala wa Trump unataka ushirikiano wa China katika kukabiliana na vitisho vya
mashambulizi ya kinyuklia ya Korea Kaskazini
No comments