Header Ads

‘Rushwa inarudisha nyuma mapambano dhidi ya Boko Haram’

ulimwenguni


LAGOS, Nigeria
SHIRIKA la Kimataifa la Kupambana na Rushwa la Transparency International (TI), limesema rushwa iliyokithiri kwenye Jeshi la Nigeria inafifisha juhudi za kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.

Shirika hilo limewashutumu maofisa mbalimbali wa kijeshi, kwa kutengeneza mikataba bandia ambapo wamekuwa wakiiba fedha kwa madai ya kununua vifaa muhimu.
Ripoti iliyotolewa na shirika hilo, imesema hali hiyo imelifanya Jeshi kuwa na rasimali pungufu pamoja na kutokuwa na mafunzo ya kutosha na kurudisha nyuma juhudi za kulitokomeza kundi hilo ambalo limekuwa likisumbua kwa miaka mingi ya karibuni.
Msemaji wa Jeshi, Meja Jenerali John Enenche alisema tuhuma hizo haziwahusu maofisa wa sasa Jeshi. Alisema hatua kubwa zimefanyika kuboresha mafunzo na kuinua ari kwa vikosi vya jeshi.

 

No comments

Powered by Blogger.