Kisa maepnzi; Binti wa mfalme Japan aukimbia ufalme
Uamuzi
huo wa Mako (pichani), ambaye ni mjukuu wa mfalme Akihito kukubali kuachana na ufalme, umekuja
baada ya kukubali kuolewa na Kei Komuro ambaye ni mwananchi wa kawaida nchini. Wawili
hao walipendana baada ya kukutana katika hoteli moja mwaka wa 2012.
Mwanamfalme
Mako mwenye umri wa miaka 25, atafunga ndoa na Komuro ambaye ni mwajiriwa wa kampuni
ya mawakili, ambaye pia walisoma pamoja katika chuo cha Christian University
mjini Tokyo.
Sheria
za kifalme nchini, zinamtaka mtu yeyote kutoka kwenye familia ya kifalme atakayeoana
na mtu asiyetoka kwenye kasri, aache ufalme. Ufalme wa Japan umethibitisha kuwa mipango ya
harusi inaendelea, lakini tarehe rasmi ya harusi itatangazwa baadaye.
Kwa
upande wake, Komuro amekataa kuzungumzia mipango ya harusi yao kwa kusema
kwamba; “Sio wakati mwafaka wa kuzungumza, nitasema muda ukifika.”
Hatua
hiyo imezua gumzo nchini, kuhusu urithi wa ufalme huku mfalme Akihito
akikaribia kustaafu.
Hii
siyo mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea, kwani shangazi yake Mako,
ambaye pia ni binti pekee wa mfalme akihito, Mwanamfalme Sayako, alilazimika
kuondoka kasrini baada ya kuoana na mpenzi wake mwaka wa 2005.
Alilazimika
kujifunza maisha ya kawaida, ikiwemo kuendesha gari na kufanya manunuzi ya
bidhaa za nyumba. Mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita, Mfalme Akihito mwenye umri
wa miaka 83, alidokeza kustaafu kwake kutokana na umri wake.
No comments