Polisi wengine 5 wauawa katika shambulio Kenya

NAIROBI,
Kenya
MAOFISA
watano wa polisi nchini, wameuawa baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa
barabarani Kaskazini Mashariki mwa mji wa Liboi karibu na mpaka na Somalia.
Shambulio
hilo lilitokea karibu na eneo lile lile, ambapo maofisa wengine wanne waliuawa katika
shambulio jingine la bomu siku ya Jumatano ambalo kundi la Al-Shabab limekiri
kulitekeleza.
Maofisa
wengine watano waliuawa katika mashambulio tofauti ya mabomu siku ya Jumatatu
katika kaunti Jirani ya Mandera.
Kundi la
wapiganaji wa Al-Shabab, limefanya mashambulio kadhaa nchini katika siku za
hivi karibuni. Kundi hilo lenye makao yake makuu Somalia, linaitaka Kenya
kuondoa majeshi yake yanayohudumu chini ya vikosi vya AMISOM.
Mwandishi wa
BBC, Mohammud Ali ameripoti kwamba shambulio hilo la Mandera lililenga gari la
gavana wa kaunti hiyo, Ali Roba.
Roba
alichapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook siku ya Jumatatu kwamba,
alipoteza mlinzi wake katika shambulio hilo. Ni shambulio la tatu ambalo
lilimlenga Roba katika kipindi cha siku tatu.
No comments