Polisi wamzuia kiongozi wa upinzani Afrika Kusini kuingia Zambia

LUSAKA, Zambia
POLISI
nchini, wamemzuia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance
(DA) cha Afrika Kusini, Mmusi Maimane kuingia nchini.
Maimane (pichani),
alikuwa akitarajiwa kuhudhuria kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini, Hakainde
Hichilema.
Hichilema
anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, baada ya kushindwa kutoa njia kwa msafara wa
Rais Edgar Lungu, hali ambayo inadaiwa kuhatarisha maisha ya mkuu huyo wa nchi.
Kiongozi
huyo wa upinzani nchini Afrika Kusini, amesema alilazimika kurudi nyumbani
baada ya maofisa kuingia ndani ya ndege ya Shirika la ndege la Afrika Kusini
aliyokuwa akisafiri nayo mjini Lusaka, kumvamia na kumnyang'anya simu yake.
Hata hivyo
bado hakuna taarifa zozote zilizotolewa na Serikali ya Zambia.
No comments