Njiwa adakwa akisafirisha dawa za kulevya Kuwait

KUWAIT CITY,
Kuwait
MAOFISA wa
forodha nchini, wamemkamata njiwa ambaye alikuwa amebeba dawa za kulevya katika
mkoba mdogo mgongoni.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Al-Rai, njiwa huyo alipatikana na jumla ya
tembe 178 ziliwekwa katika mfuko huo uliokuwa umepachikwa mgongoni mwake. Ndege
huyo alinaswa karibu na jumba la forodha jijini Abdali, karibu na mpaka na
Iraq.
Mwanahabari
wa Al-Rai, alisema kuwa dawa hizo za kulevya zilikuwa aina ya Ketamine,
nusukaputi ambayo pia hutumiwa kama dawa haramu katika sherehe.

Abdullah
Fahmi aliiambia BBC kwamba maofisa wa forodha walijua awali kuwa njiwa walikuwa
wakitumiwa kusafirisha dawa za kulevya, lakini hii ilikuwa mara ya kwanza kwa
ndege aina hiyo kunaswa katika harakati hizo.
Maofisa wa
utekelezaji wa sheria katika nchi nyingine, wamewahi kuripoti visa vya njiwa
waliodaiwa kutumiwa kusafirisha dawa za kulevya ya bei ghali japo kwa viwango
vidogo.
Mwaka wa
2015, askari wa magereza nchini Costa Rica walimnasa njiwa aliyekuwa amebeba dawa
za kulevya aina ya kokeni na bangi kwenye kipochi.
Na mwaka wa
2011, polisi wa Colombia walimkuta njiwa ambaye alishindwa kuruka juu ya ukuta
mrefu wa jela kwa sababu ya uzito wa mzigo wa dawa za kulevya aina ya kokeni na
bangi aliyopachikwa.
Njiwa
wametumika kupeperusha ujumbe tangu enzi za Roma, wakitumia uwezo wao wa kurudi
nyumbani walikotoka.
No comments