Polisi Uingereza walalamikia picha za mlipuko wa Manchester

LONDON, Uingereza
POLISI
nchini, wameyalaumu machapisho yaliyotolewa katika gazeti la New York Times la
Marekani juu ya picha na taarifa kutoka katika eneo ambalo shambulio la bomu
lilitokea mjini Manchester.
Maofisa wamesema
kuvuja kwa picha hizo kunaharibu uchunguzi wa polisi na kuondoa imani na
washirika wao katika masuala ya kiintelejinsia. Picha hizo zinaonesha vitu
mbalimbali ambavyo vingetumika kama ushahidi, kama vile betri na vitu vingine
vyenye muonekano wa vilipuzi.
Hata hivyo
gazeti hilo la Marekani, limejitetea juu ya picha hizo ambazo imesema
zinaashiria kuwa bomu lililotumika katika shambulio hilo kwa kiasi kikubwa
linaonekana kuwa ni la kisasa.
Waziri Mkuu,
Theresa May anatarajiwa kulipeleka suala hilo kwa Rais wa Marekani, Donald
Trump wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuia ya NATO, ambao unafanyika
leo.
No comments