Manchester United watwaa kombe la Europa
STOCKHOLM, Sweden
MANCHESTER United wamefanikiwa
kuibuka washindi wa Kombe la Europa, baada ya kuifunga Ajax Amsterdam kwa mabao
2-0 katika fainali iliyochezwa uwanja wa Friends mjini hapa.
Magoli
ya Paul Pogba na Henrick Mkhitaryan yameipa United sio tu Kombe la Europa, bali
pia nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Mapema
kabla ya mchezo huo kuanza, timu hizo mbili zilitoa heshima zao kwa watu
waliopoteza maisha katika shambulio mjini Manchester. Pia wachezaji wa
Manchester United na refa wa mchezo huo, walivaa vitambaa vyeusi mikononi kama
ishara ya heshima kwa waathirika.

Wafungaji
wa mabao ya Man United, Henrick Mkhitaryan aliyefunga bao la pili (kushoto) na
Paul Pogba (kulia) ambaye alifunga bao la kwanza wakishangilia bao la pili.
Anayewakimbilia nyuma ni Chris Smalling
Wakicheza
bila ya mfungaji bora wao Zlatan Ibrahimovic, pamoja na mabeki Marcos Rojo, na
Luke Shaw, pamoja na Erick Bailly anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu, kikosi
cha Mourinho kililazimika kujituma kwenye mchezo huu wa 64 msimu huu.
Wakitumia
uzoefu, pamoja na namna walivyojipanga, Man United waliweza kukisumbua kikosi
cha Ajax ambacho kilikuwa na wachezaji chipukizi, wakiwa na wastani wa umri wa
miaka 22.
Manchester
United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza
Klabu Bingwa Ulaya. Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban pauni
milioni 50.
Hili
ni kombe la pili kwa Mourinho kushinda akiwa na United katika msimu wake wa
kwanza. United walishinda Kombe la Ligi mwezi Februari mwaka huu.
No comments