Uongozi Yanga wakataa ombi la Manji kujiuzulu
Katibu
Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa
UONGOZI wa klabu ya Yanga
umethibitisha kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuf Manji alieamua
kujiweka pembeni ndani ya klabu hiyo baada ya kuiongoza kwa kipindi cha miaka
11.
Mjumbe wa kamati ya
utendaji ya Yanga, Siza Lymo alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi bado
wanashindwa kulitolea ufafanuzi zaidi kwani kwao wamepatwa na taharuki juu ya
jambo hilo.
Alisema kwamba kwa upande
wao bado hawajaridhia jambo hilo na kama kamati ya utendaji wapo katika mkakati
wa kwenda kwa mwenyekiti kumuomba ili abatilishe uwamuzi wake.
Aidha kwa upande mwingine
kiongozi wa matawi ya klabu ya Yanga, Bakili Makele alisema kwamba hapo kesho
wanataraji kuwa na kikao cha viongozi wa matawi ili kulijadili swala hilo kwa
undani zaidi.
Makele alisema kwamba
licha ya kuandika barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo lakini hiyo haiwezi
kuwa sababu ya kukaa kimya kwani bado wanamuhitaji Manji na watafanya jitihada
kubwa ili aendelee na majukumu ya klabu.
No comments