Everton kufanya ziara Tanzania

LIVERPOOL, Uingereza
KLABU ya Everton,
itazuru Tanzania kwa mechi za kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18.
Kulingana na
tovuti rasmi ya klabu hiyo, ziara hiyo ambayo ni ya kusheherekea udhamini mpya
wa klabu hiyo na Sportpesa itakuwa na mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na
nyota wa Tanzania katika uwanja wa Taifa uliopo Dar Es salaam mnamo Julai 13,
mwaka huu.
Everton
itakuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza kucheza katika taifa hilo la
Afrika Mashariki, na itakabliana dhidi ya mshindi wa kombe hilo la Sportpesa. Michuano
hiyo utashirikisha timu kutoka Tanzania na Kenya ambazo zitatoa timu nne kila
moja wao.
Mapema mwezi
huu, Everton ilitangaza udhamini wa mamilioni ya fedha na Sportpesa ambapo jina
la kampuni hiyo ya kamari litakuwa mbele ya tisheti za mabingwa hao wa zamani
wa Uingereza kwa miaka mitano.
Tangu
kuanzishwa kwake nchini Kenya mwaka 2014, kampuni hiyo imedhamini vilabu vingi,
kuwekeza mbali na kushiriki katika kamari.
No comments