Naibu Waziri akagua ujenzi wa daraja la Kelema
Mhandisi
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Kilometa 99.35, Leornado
Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la
Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto),
akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema lenye urefu wa Meta 220 linalounganisha
wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa
mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35, Mhandisi Leornado
Licari.
Mkandarasi
wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya
usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa meta 220 wakati
alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
Mhandisi
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Kilometa 99.35, Leornado
Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo
katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
Mhandisi
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga yenye urefu wa Kilometa 88.8, Kini Kuyonza
akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akikagua
zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa Kilometa 88.8 eneo la Mlima Kolo
uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi
Mshauri wa mradi huo, Mhandisi Kini Kuyonza.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 linalounganisha wilaya ya
Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo mkoani Dodoma, mara
baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara ya Mayamaya-Mela yenye
urefu wa kilometa 99.35, Naibu Waziri huyo alisema kuwa kukamilika kwa
daraja hilo na barabara za maingilio katika daraja hilo
kutarahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani
ya Manyara na Arusha.
“Daraja hili na barabara zake ni kiungo
muhimu kati ya mkoa huu na mikoa ya Manyara na Arusha na pia
inaunganisha nchi ya Tanzania, (Cape Town) South Afrika hadi (Cairo) Misri,
hivyo kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka hapa
kuelekea maeneo mengine,” alisema Ngonyani.
Aidha, Ngonyani aliitaka kampuni
ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza daraja hilo ifikapo mwezi wa kumi
mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba ili wananchi kuweza kulitumia.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa
mradi huo, Leornado Licari, alisema kwa sasa mradi umefikia asilimia 87 ambapo
hivi karibuni wanatarajia kuweka lami.
“Nakuhakikishia kumaliza mradi huu kwa
wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache, kwa hiyo hadi kufikia
mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote,” alisema Licari.
Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya
siku moja katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja
hilo pia alikagua madaraja mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela
pamoja na ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa kilometa 88.8.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments