Header Ads

Mwandishi mfichuzi wa magenge ya mihadarati auawa Mexico



Javier Valdez ameripoti pakubwa dhidi ya magenge ya ulanguzi wa mihadarati Mexico
SINALOA, Mexico
MWANDISHI habari aliyeshinda tuzo nyingi kuhusiana na taarifa zake za ufichuzi wa shughuli za makundi, yanayojihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini, ameuwawa.

Javier Valdez, aliuwawa na watu wenye silaha ambao walimiminia gari lake risasi akiwa katika mji wa Culiacán jimboni hapa Kaskazini mwa nchi.
Valdez (pichani) aliuwawa alipokuwa akiliendesha gari lake kwenda ofisini, kuliko na mtandao wake wa habari alilolianzisha huko Rio Doce.  Mfichuzi huyo aliwahi kufanya kazi katika Shirika la Habari la AFP na gazeti maarufu nchini La Jornada.
Rais Enrique Pena Nieto, ameamuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na kile alichosema uhalifu wa kutisha.
AFP nayo inasema kuwa Valdez alikuwa mtendaji kazi wa hali ya juu hususan katika shughuli za upekuzi dhidi ya walanguzi wa mihadarati, licha ya kufahamu kuwa alikuwa anahatarisha maisha yake.
Waandishi wanne wameuwawa nchini, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.