Header Ads

Watu 500 wauawa DRC



Hali bado sio ya utulivu katika eneo la Kasai
KINSHASA, DRC
JESHI nchini limesema kuwa zaidi ya watu 500 wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya usalama na vile vinavyoipinga Serikali tangu mwishoni mwa Machi mwaka huu.

Takriban wanajeshi 400 kati ya waliouawa ni wafuasi wa Kamwina Nsapu, kundi ambalo linashambulia vitu vyote vinavyohusiana na Serikali. Wanaosalia ni wanajeshi wa Serikali na polisi.
Zaidi ya watu milioni moja wameyahama makazi yao katika mkoa wa Kasai, tangu kuanza kwa mapigano hayo miezi tisa iliyopita. Zaidi ya makaburi ya pamoja 40 yamekutwa katika eneo hilo.

No comments

Powered by Blogger.