Header Ads

Marekani yaituhumu Syria kwa kuchoma wafungwa gerezani



Picha ya gereza hilo iliyopigwa kwa Satelite 

Picha ya gereza la kijeshi iliyopigwa kwa satalaiti. Syria imejenga kujenga sehemu ya kuchomea maiti karibu na gereza hilo, lakini inadaiwa kuitumia kuchoma wafungwa.
WASHINGTON DC, Marekani
MAREKANI imeituhumu Serikali ya Syria, kwa kujenga sehemu ya kuchoma maiti katika jela ya kijeshi iliyopo karibu na Damascus ili kuficha mauaji ya halaiki ya watu wanaoshikiliwa na Serikali.

Wizara ya Mambo ya Nje, imeonesha picha zilizopigwa kupitia njia ya Satalaiti ambazo imesema ni sehemu ya kuchoma maiti katika gereza lililopo Sednaya ambapo Umoja wa Mataifa (UN) na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema maelfu ya wafungwa wameteswa na kunyongwa.
Mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani anayehusika na masuala ya Mashariki ya kati, Stuart Jones, amesema kwa siku wafungwa takriban 50 wanauawa katika gereza la Sednaya.
Ameongeza kusema kuwa, mauaji hayo yanafanyika kutokana Syria kuungwa mkono na Urusi na Iran.

No comments

Powered by Blogger.