Mke wa Hichilema aomba Zambia imwachie mumewe
Hakainde Hichilema
LUSAKA,
Zambia
MKE wa kiongozi
mkuu wa upinzani nchini, Hakainde Hichilema, ametoa mwito kwa jamii ya
kimataifa kusaidia kuachiwa kwa mumewe.
Mutinta
Hichilema alisema kuwa kudorora kwa demokrasia nchini, na nchi kutumbukia
kwenye utawala wa kiimla ni jambo ambalo haliwezi kupuuzwa.
Alitoa
matamshi hayo wakati Serikali ya Uingereza iliposema kuwa, wawekezaji wanatiwa
hofu na kuendelea kuzuiwa kwa Hichilema kutokana na mashtaka ya uhaini.
Jana Jaji
mmoja anayesikiliza mashitaka yanayomkabili Hichilema, alitarajiwa kuamua ikiwa
kesi hio itatupiliwa mbali au ipelekwe kwenye mahakama ya juu. Mashtaka hayo
yanatokana na kile kinachotajwa kuwa hatua ya Hichilema kuzuia msafara wa
magari ya Rais.
No comments