Korea Kaskazini yakiri kufanyia majaribio kombora lingine
Kombora la Pukguksong 2 lilipofanyiwa majaribio jana
PYONGYANG,
Korea Kaskazini
KOREA
Kaskazini imekiri kuwa imefanikiwa kwa mara nyingine, kurusha kwa mafanikio kombora
la masafa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari nchini (KCNA), ilieleza kuwa
kombora hilo lililojaribiwa Jumapili kwa sasa liko tayari kwa ajili ya matumizi
ya kijeshi.
Ikulu ya
White House ya Marekani, ilisema kuwa kombora hilo lilikuwa la masafa marefu
kuliko makombora yaliyotumiwa na Korea Kaskazini wakati majaribio matatu ya
awali.
Jaribio hilo
linakuja wiki moja baada kufanyika kwa majaribio mengine, yaliyotajwa kuwa makombora
mapya yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.
Jumatatu
iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilisema kuwa Korea haistahili
kufanya majaribio zaidi. Sasa baraza hilo linatarajiwa kukutana kwa faragha leo
kwenye mkutano ulioitishwa na Marekani, Korea Kusini na Japan.
Kiongozi wa taifa,
Kim Jong-un alishuhudia shughuli ya jaribio la kombora la Pukguksong-2 jana. Wizara
ya Mashauri ya Nje ya Korea Kusini, imelitaja jaribio hilo kuwa la kiholela
huku Waziri wa Mashauri ya Nje wa Marekani akilitaja kuwa la kughadhabisha.
Kombora hio
lilisafiri umbali wa kilomita 560 kuelekea bahari ya Japan. Kombora la wiki
iliyopita lilisafri umbali wa kilomita 700.
No comments