Watu 141 kwa kuhudhuria sherehe ya wapenzi jinsia moja
JAKARTA, Indonesia
POLISI
nchini, wamewakamata wanaume 141 ambao walikuwa wanahudhuria sherehe ya wapenzi
wa jinsia moja ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini hapa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na polisi, sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili, ilikuwa
na kiingilio cha Rupia 185 (dola 14 za Marekani) lakini waliishia kukamatwa
kutokana na vitendo hivyo.
Taarifa hiyo
ilieleza kwamba, pamoja na watu waliokamatwa alikuwepo raia mmoja wa Uingereza.
Katika siku za karibuni, Indonesia imeshuhudia kuongezeka kwa chuki kwa dhidi
ya wapenzi wa jinsia moja.
Mapenzi kati ya watu wa jinsia moja sio marufuku
kulingana na sheria za Indonesia, isipokuwa katika mkoa wa kihafidhina wa Aceh.
Lakini Msemaji wa Polisi wa Jakarta, Raden Argo
Yuwono alisema baadhi ya wale walio kizuizini wanaweza kushtakiwa chini ya
sheria kali ya Indonesia ya kupambana na vitendo vichafu.
“Baadhi yao walipatikana wakiwa wamevua nguo na
wakishiriki ngono na wengine kujipiga punyeto wakati wa tukio,” aliiambia idhaa
ya BBC Indonesia.
Chini ya sheria hizo kali za Indonesia, kuandaa onesho
kama hilo ili kuwatumbuiza watu inaweza kufasiriwa kama kosa la kutenda kitendo
kichafu eneo la umma.
Wiki iliyopita, wanaume wawili walihukumiwa
kuchapwa viboko mbele ya umma katika mkoa wa Aceh, baada ya kupatikana
wakifanya ngono. Sheria kali dhidi ya uhusiano wa kimapenzi kati ya watu wa
jinsia moja, zilianza kutekelezwa nchini mwaka 2014.
Mapema mwezi huu, polisi waliwatia mbaroni watu 14
katika mji wa Surabaya.
BBC
No comments