Korea Kaskazini: Mazingira yakiruhsu tutazungumza na Marekani
SEOUL, Korea
Kusini
KOREA
Kaskazini imesema kuwa itafanya mazungumzo na Marekani iwapo mazigira
yataruhusu, kulingana na taarifa ambayo imeripotiwa na vyombo vya habari nchini.
Mjumbe Mwandamizi
wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui (pichani) alisema kuwa mazungumzo na Marekani
yanawezekana kufuatia mkutano na waliokuwa maofisa wa Serikali ya Marekani
nchini Norway.
Awali mwezi
huu, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema itakuwa heshima kubwa kukutana na Rais
Kim Jong un. Matamshi yake yalijiri kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi
kuhusu mipango ya Korea Kaskazini ya kinyuklia, pamoja na ile ya utengezaji wa
makombora ya masafa marefu.
Hui ambaye
ni ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu masuala ya Marekani Kaskazini,
alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akirudi Pyongyang baada ya mkutano mjini
Oslo.
No comments