Video ya Boko Haram yaonesha wasichana waliokataa kuachiwa
Wiki
iliyopita, wasichana 82 kati yao waliachiliwa huru baada ya miaka miwili wakiwa
chini ya watekaji wao. Waliachiwa baada ya Serikali kuwaachia makamanda watano
wa Boko Haram.
Kwa
sasa, kuna wasichana takriban 100 wa Chibok ambao bado wanashikiliwa na wapiganaji
hao huku Serikali ikisema kuwa mazungumzo ya kuwasihi Boko Haram kuwaachia huru
yanaendelea.
Mmoja
ya wasichana hao alionekana akibeba bunduki, huku mwingine akisema kuwa asingependelea
kurudi nyumbani kwa sababu familia yake haiwezi kubadilika na kuwa Waislamu.
Wasichana
82 walioachiwa wiki iliyopita wanasubiri kuunganishwa na familia zao, lakini
wataendelea kuwa chini ya uangalizi maalum wa Serikali.
Msemaji
wa Ofisi ya Rais nchini, alisema kuwa msichana mwingine alitarajiwa kuachiliwa
lakini akakataa. Inadaiwa kuwa wasichana wengine waliolewa na watekaji hao na kupata
watoto.
BBC
No comments