Trump aunga mkono mpango wa nyuklia wa Iran

Rais wa Marekani, Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari ikulu leo.
WASHINGTON
DC, Marekani
IKULU ya
Whitehouse nchini, imeendeleza mpango wa kuipunguzia vikwazo Iran licha ya Rais
Donald Trump kuukosoa mpango huo.
Kuondolewa
kwa vikwazo ni miongoni mwa makubaliano ya kinyuklia yalioafikiwa mwaka 2015,
chini ya Rais mstaafu, Barrack Obama pamoja na mataifa mengine matano yenye
uwezo mkubwa duniani.
Trump
ameelezea makubaliano hayo kuwa mabaya zaidi. Hatahivyo, Wizara ya Fedha nchini
iliwawekea vikwazo maofisa fulani na mfanyibiashara wa China anayehusishwa na
mpango wa makombora wa Iran.
Hatua hiyo
inamaanisha vikwazo vinavyozuia kampuni zozote za Marekani zinazoiuzia ama
kushirikiana na Iran vitaendelea kulemazwa.
Kwa upande
wake, Iran imekubali kupunguza mipango yake ya nyuklia, kupunguza uhifadhi wa
madini ya Uranium, uzalishaji wa Plutonium na kuwaruhusu wachunguzi kuchunguza
vifaa vyake.
Vikwazo
vipya kutoka kwa Wizara ya Fedha vinaathiri watu binafsi wakiwemo maofisa
wawili wa Iran, katika idara ya ulinzi na wanaouza makombora ya kijeshi ili
kulipiza kisasi jaribio la kombora pamoja na hatua ya Iran kumuunga mkono,
Bashar al-Assad wa Syria.
Raia wa
Marekani na washirika wake sasa hawaruhusiwi kuingia mikataba na maofisa hao na
kampuni husika.
No comments