Kisa albamu, Kanye afuta akaunti zake
BAADA ya kufuta
akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na twitter, Kanye West anatarajia
kuachia album yake.
Album hiyo imeanza
maandalizi ambayo mpaka sasa ni wiki mbili tangu rapa huyo aamue kujitenga na
kuhamia sehemu za milima. Watu wameanza kuhisi huenda wawili hao, yaani Kim na
Kanye wamegombana ndio maana Kanye hakuonekana wiki iliyopita katika usiku wa
Met Gala na baby mama wake Kim kama ilivyo kawaida ya wawili hao.
Mara ya mwisho kwa
wawili hao kuonekana kwa pamoja ilikuwa kwenye chakula cha usiku wakati wa
Valentine. Kanye hajaonekana hata kwenye uzinduzi wa mavazi yake ya Yeezy. Na
mpaka sasa hajawahi kufanya show yoyote tangu alipotoka hospitali mwaka jana
Novemba.
No comments