French Montana amwaga noti Uganda
Mwanamuziki kutoka
Marekani mwenye asili ya Morocco, Karim Kharbouch a.k.a French Montana (pichani) ametoa
msaada wa dola za Marekani, 100,000 (sawa na shilingi milioni 220 za Bongo) Uganda.
Montana ametoa msaada
huo kwa taasisi ya Mama Hope nchini humo, pia ameanzisha kampeni inayojulikana
kama Unforgettable Dance Challenge yenye lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya
kusaidia jamii kuondokana na umaskini.
Montana amenukuliwa
akisema, “Muda mwingine Mungu anakupa uwezo wa kuwa sehemu fulani ili uwasaidie
na watu wengine. Nataka niwape kile nilichonacho na kuwasaidia haraka
iwezekanavyo.”
Kwa sasa Unforgettable
ndio ngoma mpya ya msanii huyo aliyofanya Uganda na kushirikisha dance wa
vijana Ghetto wa Uganda.
No comments