Kirusi cha WannaCry chahusishwa na Korea Kaskazini
Mfanano wa
nambari maalum za mawasiliano (codes), baina kirusi cha WannaCry na kirusi
kingine kilichotumika mwaka 2014 kuishambulia kampuni ya filamu ya Sonny Pictures.
Mfanano huu umegunduliwa na mtaalam wa kompyuta wa Google, Niran Mehta
LONDON,
Uingereza
NANI
alihusika katika shambulio la kirusi cha mtandaoni ambacho kiliathiri kompyuta
katika zaidi ya mataifa 150 duniani, zikiwemo Kenya na Tanzania? Kumeibuka
madai kwamba huenda wadukuzi walitoka Korea Kaskazini.
Lakini
kufikia sasa, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha hilo.
Huenda
hujawahi kusikia kuhusu kundi linaloitwa Lazarus Group, lakini pengine
unafahamu baadhi ya matokeo ya shughuli zake. Kundi hili lilihusika katika
kudukua mfumo wa kompyuta wa Sony Pictures mwaka 2014 na tena wakadukua benki
moja ya Bangladesh mwaka 2016.
Inasadikika
kwamba wadukuzi hao wa Lazarus Group walifanyia kazi yao China lakini kwa niaba
ya Korea Kaskazini.
Wataalamu wa
usalama mitandaoni. sasa wanahusisha shambulio la kirusi cha WannaCry na kundi
hilo baada ya ugunduzi uliofanywa na mtaalamu wa usalama wa kompyuta wa Google,
Neel Mehta.
Mehta
aligundua kwamba, maelezo ya kutunga programu ya kompyuta ya kirusi cha
WannaCry yanafanana na maelezo ya programu zilizowahi kutumiwa na Lazarus Group
awali. Huenda ikawa labda ni sadfa tu, lakini kuna viashiria vingine. Kutofautisha
maelezo ya kompyuta
Profesa Alan
Woodward, mtaalamu wa usalama wa mifumo ya kompyuta, anasema ujumbe wa kuitisha
kikombozi unatumia lugha inayoonekana kana kwamba aliyetafsiri alitumia
kompyuta kuufanya kuwa wa Kiingereza, na ujumbe ulioandikwa kwa Kichina
unaonekana kuandikwa na Mchina asilia.
“Mnavyoona
uhusiano ni mdogo sana na labda ni sadfa tu,” Prof Woodward alisema
Hata hivyo,
uchunguzi zaidi unahitajika. “Ugunduzi wa Neel Mehta ndiyo kiashiria muhimu
zaidi kufikia sasa, kuhusu chanzo cha WannaCry,” kampuni ya usalama wa kompyuta
ya Urusi, Kaspersky, ilisema.
Hata hivyo,
maofisa hao wanasema habari zaidi zinahitajika kuhusu aina za awali za WannCry
kabla ya uamuzi kamili kufanywa.
“Tunaamini
kwamba ni muhimu watafiti wengine maeneo mengine ya dunia wachunguze kuhusu
kufanana huku, na wajaribu kuchimba zaidi kupata maelezo zaidi kuhusu asili ya
WannaCry,”
“Ukiangalia
shambulio la udukuzi la benki hiyo ya Bangladesh, siku za mwanzo, hakukuwa na
maelezo mengi ya kulihusisha na kundi la Lazarus Group.
“Baadaye,
ushahidi zaidi ulitokea na kutuwezesha, pamoja na wengine, kuhusisha kundi hilo
na shambulio hilo kwa imani zaidi. Utafiti zaidi unaweza kuwa muhimu sana
katika kubainisha ukweli,” alisema Profesa Woodward
Huwa vigumu kubaini
nani amehusika katika shambulio la mtandao na mara nyingi hutegemea maafikiano
badala ya uthibitisho.
Kwa mfano,
Korea Kaskazini haijawahi kukiri kuhusika katika udukuzi wa Sony Pictures na
ingawa watafiti, na Serikali ya Marekani, wanaamini kwamba ni Korea Kaskazini
iliyohusika, hakuna anayeweza kupuuzilia mbali uwezekano kwamba madai hayo si
ya kweli.
Wadukuzi
walio na utaalamu wa juu wanaweza kuifanya ionekane kwamba shambulio hilo
lilitoka Korea Kaskazini kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Ushahidi
hauwezi kujisimamia' Kuhusu WannaCry, kuna uwezekano kwamba wadukuzi walinakili
tu maelezo ya kompyuta yaliyotumiwa awali na Lazarus Group.
Lakini
Kaspersky wanasema dalili za kupotosha katika maelezo ya WannaCry zinaweza
kuwepo lakini ni vigumu kiasi, kwani katika toleo la baadaye la kirusi hicho,
maelezo yaliyokuwa yanafanana na ya Lazarus Group yaliondolewa.
"Kuna
shaka sana. Kwa sasa ni kwamba ushahidi uliopo hauwezi kujisimamia kortini. Ni
muhimu kuchunguza zaidi, kwa kutilia maanani pia mtazamo wa wengi kwa sasa
kuhusu Korea Kaskazini, jambo ambalo huenda linaongoza uamuzi wa wengi,” alisema
Profesa Woodward.
Kadri dalili
zilivyo kwamba Korea Kaskazini huenda ilihusika katika kuunda WannaCry, kuna
pia dalili za kuonesha labda Korea Kaskazini haikuhusika.
Mwanzo,
China ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo ziliathirika pakubwa kutokana na wadukuzi
walihakikisha kwamba kulikuwa na nakala ya ujumbe wa kuitisha kikombozi
ulioandikwa kwa Kichina. Ni vigumu kwa Korea Kaskazini kuwa ilitaka kuudhi
mshirika wake mkuu China. Urusi pia iliathirika sana.
Pili,
mashambulio ya mtandao ya Korea kaskazini, sana hulenga asasi fulani, na huwa
na lengo la kisiasa.
Kuhusu Sony
Pictures, wadukuzi walitaka kuzuia kutolewa kwa filamu ya The Interview,
iliyomtania kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un. Kwa WannaCry, hali
ilikuwa kinyume, kirusi hicho kilikuwa kinaambukiza kompyuta yoyote ile
iliyokuwa haijalindwa vyema.
Mwisho
kabisa, iwapo mpango ulikuwa kuunda pesa, haujafanikiwa kwani ni
$60,000 (sh
milioni 122) pekee zimelipwa kama kikombozi, kwa mujibu wa akaunti za Bitcon
zinazotumiwa na wadukuzi hao.
Ikizingatiwa
kwamba ni kompyuta zaidi ya 200,000 zilizoathiriwa, kiasi hicho cha pesa ni cha
chini mno. Lakini pengine kikombozi hicho kiliwekwa kuficha lengo la kisiasa.
Kuna
uwezekano pia kwamba Lazarus Group walifanya kazi kivyao bila kuagizwa na Serikali
ya Korea Kaskazini na pia yawezekana kuwa Lazarus Group hawana uhusiano na Korea
Kaskazini. Kwa sasa, kuna maswali mengi yasiyo na majibu.
No comments