Upinzani watishia kususia uchagui Kenya
Viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani Kenya (NASA) wakiimba wimbo kwa pamoja katika moja ya mikutano yao. Viongozi hao wametishia kususia uchaguzi.
NAIROBI,
Kenya
MZOZO mpya
umeibuka kati ya Tume Huru ya Uchaguzi nchini (IEBC), na vinara wa mrengo wa
upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.
IEBC
imeijibu Nasa, kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo
itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama
ulioruhusu matokeo ya kura za urais kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.
Hii ni baada
ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC, kusaka njia za kubadili mipango hiyo
ili kutangaza matokeo ya kura za urais katika kituo cha kitaifa jinsi
ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.
Tume hiyo
kupita mwenyekiti wake, Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitabadili msimamo
wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu mahakama na
kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.
Viongozi wa upinzani
wakiongozwa na mgombea wa urais, Raila Odinga, walitishia kususia uchaguzi
iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu matokeo ya Urais kutoka kila kituo
kutangazwa kitaifa.
“Kuitishia
IEBC kuhusu uamuzi wake wa kukata rufaa, ni kutishia uhuru wake, na
wasioridishwa na hatua hiyo, wajiunge kwenye kesi wasake suluhisho za kisheria,”
alisema Chebukati.
Kenya inatarajiwa
kuandaa uchaguzi mkuu wa urais baadaye mwaka huu, huku ushindani mkali
ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia mrengo
wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa Upinzani wa
Nasa. Takriban wagombea 18 wa urais
wamejitokeza.
No comments