Header Ads

Mashambulizi ya kompyuta kuathiri watu kuanzia kesho



Udukuzi wa komputa kuathiri watu zaidi Jumatatu
Mdukuaji
LONDON, Uingereza
WATAALAMU wa usalama katika mitandao ya kompyuta, wameonya kwamba kunaweza kukatokea mashambulio mengine sehemu mbalimbali za dunia, pale watu watakaporudi kazini hapo leo.

Inakisiwa kuwa kompyuta zaidi ya 120 katika nchi kama 100, zilidukuliwa mwishoni mwa wiki. Lakini polisi wa Umoja wa Ulaya, wamesema walioathirika na udukuzi huo ni watu 200,000 katika mataifa 150.
Shambulio hilo limeathiri watumiaji pamoja na ofisi za serikali, kampuni zinazotengeneza magari, benki na huduma za afya. Shambulio hilo limezuia kompyuta kufikia takwimu, na wanadai kikombozi, ili kuiachia kompyuta.
Uchambuzi uliofanywa na BBC katika akaunti tatu za sarafu ya kidijitali, bitcoin, unaonyesha washambuliaji wamelipwa kikombozi zaidi ya mara 100, jumla ya dola karibu 30,000 (sh milioni 66).

No comments

Powered by Blogger.