Ujerumani yaipiga England 1-0
BERLIN, Ujerumani
TIMU ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao
1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo liliwekwa
kambani na mshambuliaji Lukas Podolski (pichani) katika dakika ya 69 ya mchezo kwa shuti
kali la umbali wa mita 25 lilomshinda kipa wa England Joe Hart.
Mchezo huu wa kirafiki ulikua ni mchezo wa mwisho
kwa mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ujerumani, anayestaafu soka la
kimataifa akiwa na umri wamiaka 31.
No comments