Daktari wa maradhi ya moyo Mtanzania apata tuzo
MOROGORO,
Tanzania
DAKTARI Mshauri
Mwandamizi wa magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani hapa, Dk Harun
Emalda Nyagori (pichani) amepewa tuzo na Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo Marekani
(American college of Cardiology).
Dk Nyagori
ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis, amepewa tuzo ya
kutambuliwa kwa utafiti na uzoefu wake katika ushauri kuhusu magonjwa ya moyo
barani Afrika.
Baadhi ya
utafiti uliofanywa na Dk Nyagori ni pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa dawa
za maradhi ya moyo nchini na changamoto za magonjwa ya moyo hapa nchini.
Tuzo
nyingine alizopata ni kutoka kwa Jumuiya ya Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo
barani Ulaya na Jumuiya ya Umoja wa Madaktari bingwa wa maradhi ya moyo nchini
Mexico.
Dk Nyagori
ni kati ya madaktari bingwa wachache nchini wanaoshauri na kutibu maradhi ya
moyo yasiyohusiana na upasuaji. Amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka saba sasa
akiwasaidia wangonjwa katika mkoa wa Morogoro na mikoa jirani inayopakana na
Morogoro.
Dk Nyagori
pia aliwahi kupokea tuzo nyingine. Septemba 2015 alipokea tuzo kutoka Jumuiya
ya Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo Barani Ulaya, London. Tuzo nyingine ni
kutoka Jumuiya ya Umoja wa madaktari bingwa wa maradhi ya Moyo nchini Mexico
mwaka 2016.
Kwa
kushirikiana na madaktari wengine, Dk Nyagori amekuwa akiwatibu kwa wastani
wagonjwa 40 hadi 60 kwa siku. Idadi inayofikia wastani wa wagonjwa 160 - 200
kwa wiki.
No comments