Sarafu ya dhahabu yenye thamani kubwa yaibiwa Ujerumani
Picha
ya sarafu hiyo ya dhahabu iliyoibiwa. BBC
BERLIN,
Ujerumani
SARAFU kubwa
ambayo imetengenezwa kwa dhahabu, ikiwa na picha ya Malkia Elizabeth wa
Uingereza, inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 4 (sh
bilioni 8.8), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho nchini.
Sarafu hiyo
kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu
imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu kulingana na bei
ya sasa ya dhahabu.
Iliibiwa
usiku kutoka makavazi ya Bode mjini Berlin. Haijabainika ni vipi wezi
walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha kutoroka
na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.
Wizi huo
unaaminika kutekelezwa mwendo wa saa tisa unusu alfajiri ya jana Jumatatu. Sarafu
hiyo inadaiwa kuwa nzito kiasi kwamba mtu mmoja hawezi kuibeba. Polisi wa eneo
hilo wanasema huenda wezi hao waliingia kupitia dirisha.
Ngazi
ilipatikana imetupwa kwenye reli iliyo karibu, msemaji wa polisi Winfrid Wenzel
aliambia Reuters.
“Sarafu hiyo
ilikuwa imehifadhiwa ndani ya sehemu isiyoweza kupenya risasi ndani ya
makumbusho,” alisema.
Sarafu hiyo
ilifuliwa mwaka 2007 na Royal Canadian Mint.
No comments