Header Ads

Canada kuhalalisha bangi mwakani

https://files.merryjane.com/uploads/article/small_image/1250/MAKE_MARIJUANA_GROWING_A_GREENER_OPERATION_WIDE.jpg

OTTAWA, Canada
MATUMIZI ya bangi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini, ifikapo tarehe mosi Julai 2018.
Serikali imeeleza kuwa itawasilisha muswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la Serikali la CBC.

Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi karibuni, walijulishwa kuhusu muswada huo. CBC ilisema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na Serikali.
Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa, Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi kwa ajili ya watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18 kujiburudisha. Jopo kazi hilo, pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na kumiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa.
Kwa mujibu wa CBS, Serikali itasimamia kusambazwa kwa bangi na kuwapa leseni wazalishaji.
Ahadi wa Waziri Mkuu, Justin Trudeau ya kuhalalisha bangi imechochea uvumi katika sekta hiyo.
Wazalishaji kama kampuni ya Aphria, OrganiGram Holdings, na Canopy Growth, ambao ni wazalishaji wakubwa zaidi wa bangi ya kutibu, yamekuwa vipnzi kwa wawekezaji wa hisa.




 

No comments

Powered by Blogger.