Maneno ya kibaguzi yamponza raia wa Ujerumani
Lilongwe,
Malawi
RAIA mmoja wa
Ujerumani ambaye anafanya kazi nchini, Hinteregger Jurgen anakabiliwa na hati
hati ya kurudishwa nchini kwao baada ya kudaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi kwa
mmoja wa wafanyakazi aliokuwa akiwasimamia.
Kwa mujibu
wa gazeti la Nyasa Times, inadaiwa kuwa Jurgen alimwita ‘nyani’ dereva wake
ambaye alikuwa akiendesha gari lililobeba maji baada ya kushindwa kulihimili na
kugonga vizuizi na kupasuka tairi.
Msemaji wa
Polisi nchini, Ignatius Easu alisema kuwa mara baada ya tukio hilo Jurgen
ambaye anasimamia ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 47 aliteremka kwa
hasira na kusikika akimwita ‘nyani’ dereva huyo kisha kumpokonya funguo za gari
hilo.
Mara baada
ya kukamatwa na polisi, Jurgen alipelekwa katika kituo cha polisi cha Songwe
kilichopo mpakani mwa Malawi na Tanzania, ambapo aliwekwa mahabusu kabla ya
kuletwa jijini hapa kwa ajili ya hatua nyinginezo.
Maneno hayo
ya kibaguzi yaliyotolewa na msimamizi huyo, yalisababisha mgomo mkubwa wa
wafanyakazi ambao walidai kuwa wanagoma kwa lengo la kumuunga mkono mfanyakazi
mwenzao aliyedhalilishwa.
No comments