Watoto 30 wafariki kwa kukosa hewa India

UTTAR PRADESH- WATOTO wachanga
30 wamefariki dunia katika hospitali moja jimboni hapa, baada ya kukosa hewa ya
oksijeni ambayo ilikuwa ikiwasaidia kupumua.
Upungufu
wa hewa hiyo muhimu kwa vichanga vilivyozaliwa kabla ya muda, ulitokana na
hospitali hiyo kudaiwa fedha nyingi na wazabuni wanaosambaza bidhaa hiyo
hospitalini hapo.
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini, aliliambia shirika la habari la Press Trust
la India kuwa, ni watoto 21 ndiyo waliofariki kutokana na tatizo hilo la
ukosefu wa hewa ilhali wengine walifariki kutokana na vifo vya kawaida.
Kwa
mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio, matenki ya kutunzia hewa hiyo
yaliishiwa oksijeni na kusababisha vifo hivyo na kusababisha matabibu kuanza
kuwapatia wazazi mabegi maalum ya kupumulia ili kuwaokoa watoto wao.
“Tulishuhudia
watoto waliokuwa wakituzunguka wakipoteza maisha. Kwa kawaida, ni kosa la
hospitali. Watoto wengi walifariki dunia kwa sababu ya uzembe wao. Mwanangu alikuwa
mzima hadi kufikia usiku, wakati tuko baya lilipomfika,” alisema mmoja wa
wazazi ambaye alijitambulisha kwa jina la Vijay.
Independent.
No comments