Tetesi Asubuhi; Chelsea wamnyatia Perisic # Griezman aitaka Man Utd # Liverpool wamtaka Insigne
LONDON- BAADA ya kukumbana na kipigo cha bao 3-2
wikiendi hii, Chelsea
wamepanga kumnyakua winga wa Inter Milan, Ivan Perisic (28) ambaye ni windo la muda
mrefu la Man United. Mirror.
Mshambuliaji
mahiri wa Atletico Madrid, Antoine Griezman (26) amesema ataangalia uwezekano
wa kujiunga na Man United, endapo timu yake itaamua kumuuza kipa wao, Jan Oblak
kwenda PSG. Hatua hiyo imeelezwa kutomfurahisha Mfaransa huyo. Don Ballon.

Manchester
United wamesema watakuwa tayari kutoa pauni milioni 36.5 (sh bilioni 105.8), kama
ada ya kumnunua kiungo wa Barcelona, Sergi Roberto (25) endapo mchezaji huyo
atasisitiza kuondoka Nou Camp. Don Ballon.

Kocha
wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema timu hiyo inatakiwa kufanya usajili kabla ya
dirisha la usajili kufungwa, ili kuimarisha kikosi chao. Pia, Klopp amesema
anamtaka Lorenzo Insigne (26) wa Napoli, ili kuziba pengo la Philippe Coutinho
anayekwenda Barcelona. Express.

Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Juventus, Beppe Marotta amesema timu hiyo inavutiwa na windo
la Liverpool linalokipiga RB Leipzig, Naby Keita (22). La Gazzetta dello Sport.
Beki
wa Chelsea, Cesar Azpilicueta (27) amesema kuwa timu hiyo inahitajika ifanye
usajili haraka kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili ili kukiimarisha kikosi
chao kinachoonekana kuwa kidogo. Evening
Standard.

Tottenham
wamesema wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Lazio, Keita Balde (22),
baada ya mchezaji huyo kuachwa nje ya kikosi kilichocheza jana dhidi ya
Juventus kwenye kombe la Supercoppa Italiana. Mirror.
Chelsea
imesema iko tayari kutoa dau la pauni milioni 50 (sh bilioni 145), kwa ajili ya
kumsajili beki wa Southampton anayewindwa na Liverpool, Virgil van Dijk (26). Daily Star.
Manchester
United wameeleza kuwa wamekaribia kuelewana maslahi binafsi na mshambuliaji
kinda wa Oliveirense ya Ureno, Bruno Amorim (19). Daily Mail.
Leicester
City imesema itakataa dau la pauni milioni 31.8 (sh bilioni 92.2), ambazo
zitatolewa na AS Roma ya Italia, kama dau la usajili la Riyad Mahrez (26).
Leicester wanataka pauni milioni 50 (sh bilioni 145). Mirror.
Kocha
wa Everton, Ronald Koeman amesema hataweza kuvumilia kuona kiungo wa timu hiyo,
Gareth Barry (36) akiondoka klabuni hapo kwenye dirisha hili la usajili.
Liverpool Echo.
Kocha
wa Swansea, Paul Clement amekitaka chama cha soka Uingereza (FA), kiweke
utaratibu wa kufungwa kwa dirisha la usajili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa
Ligi Kuu. Kwa sasa, Clement anapambana kumbakiza kiungo Gylfi Sigurdsson (27).
Daily Mail.
Newcastle
United imeongeza juhudi za kumnasa kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere (25), baada
ya mchezaji huyo kuachwa kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Leicester City. Sun.
No comments