Scaramucci: Kuna watu wanataka kumng’oa madarakani Trump

NEW YORK-
OFISA wa Mawasiliano ambaye alidumu kwa muda mfupi katika ikulu ya Marekani,
Anthony Scaramucci amesema kuna watu ndani ya Serikali ambao wanataka kumng’oa
madarakani Rais Donald Trump.
Akizungumza
na televisheni ya ABC, alisema Trump analengwa kwa sababu hakuwamo kati ya
viongozi wa siasa nchini humo. Alipoombwa ataje majina, Scaramucci alisema
ameshawataja na rais anahitaji kuleta watu zaidi walio watiifu kwake.
Alipohudumu
kwa siku kumi, Scaramucci alikosoa watu kadhaa pamoja na mkuu wa ofisi ya rais
wa zamani, Reince Priebus.
BBC
No comments