Mwenyekiti IEBC asema matokeo ya wapinzani hayaeleweki

NAIROBI-
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC), Wafula Chebukati amesema tume
hiyo ilipokea barua kutoka kwa muungano wa upinzani (NASA) ambapo wanadai
mgombea wao Raila Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne.
Chebukati
amesema matokeo hayo hayaeleweki, kwa sababu muungano huo haukuambatanisha Fomu
34A za matokeo vituoni ambazo walitumia kufanya hesabu yao.
Aidha,
ameongeza kuwa muungano huo unafanya makosa kwani ni kinyume cha sheria kwao
kujitangazia matokeo.
Hadi
sasa, matokeo ya awali yanaonesha Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee anaongoza
akiwa na kura 8,163,572 dhidi ya kura 6,747,099 za Raila Odinga wa chama cha
ODM kilicho katika muungano wa National Super Alliance maarufu NASA.
Matokeo
yaliyotangazwa ni ya vituo 40489 kati ya vituo 40883. Kura zilizoharibika
zimeendelea kuwa nyingi, na kufikia sasa ni kura 399 935.
BBC
No comments