Watu 40 wauawa uvamizi wa Boko Haram

MAIDUGURI- WATU
40 wameuawa, katika jaribio la kuwaokoa mateka wa kundi la wanamgambo la
Kiislamu la Boko Haram.
Takriban
watu watano wa kampuni ya kuchimba mafuta waliuawa, kwa mujibu wa chuo cha
Maiduguri.
Wanajeshi
pia waliuawa wakati wa uvamizi huo. Idadi hiyo kubwa ya vifo, ni pigo kwa Serikali
ambayo inasisitiza kuwa kundi la Boko Haram limeshindwa.
Taarifa za
kina kuhusu kile kilichotokea Jumanne hazijulikani, huku ripoti za awali kutoka
kwa jeshi, zikisema kuwa watu ambao walitekwa ni pamoja na wafanyakazi wa chuo
cha Maiduguri ambao hata hivyo waliachiwa.
Jeshi
lilisema kuwa miili ya wanajeshi 9 na raia mmoja, ilipatikana katika eneo la
tukio Jumanne.
Lakini sasa
chuo hicho kimesema kuwa, takriban wafanyakazi watano wakiwemo wasomi wawili na
dereva waliuawa wakati msafara wao uliokuwa chini ya ulinzi mkali, uliokuwa
ukirejea ulipovamiwa huku.
Takriban
watu 20,000 wameuawa na maelfu ya wengine kutekwa tangu Boko Haram ianzishe
harakati zake mwaka 2009.
Katika kisa
kibaya zaidi Boko Haram, waliteka wasichana 276 kutoka shule ya wasichana ya
Chibok iliyopo Kaskazini Mashariki mwa nchi mwaka 2014. Tangu wakati huo,
wamewaachilia zaidi ya wasichana 100 kubadilishana na wapiganaji.
BBC
No comments