Header Ads

Ukosefu wa bangi wasababisha hali ya tahadhari kutangazwa Nevada



Cannabis plant

NEVADA- MAOFISA wa Serikali jimboni hapa, wametangaza kuanza kuchukua hatua za dharura za kukabiliana na uhaba wa bangi.
Hali hiyo inatokana na mahitaji kuwa ya juu, tangu bangi ihalalishwe kwa matumizi ya kujiburudisha mwanzoni mwa mwezi huu. Uhaba huo unadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na uchache wa wauzaji wa mmea huo.
Sheria iliwapa wauzaji wa pombe ruhusa ya kuuza bangi, lakini wengi hawatimizi mahitaji ya leseni kuweza kuuza bidhaa hizo.
Idara ya kodi jimboni hapa, ilitangaza dharura inayomaanisha kuwa maofisa watachukua hatua za dharura kukabiliana na uhaba huo.
Mauzo ya karibu dola milioni 3 (sh bilioni 6.6), yalikadiriwa siku nne za kwanza baada ya matumizi ya bangi kuhalalishwa. Nevada ilipiga kura ya kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani Novemba mwaka jana, kufuatia hatua kama hizo katika majimbo mengine.
Matumzi ya bangi kwa matibabu yameruhusiwa katika majimbo 25 ikiwemo Nevada, ambapo imehalalishwa tangu nwaka 2001.
BBC

No comments

Powered by Blogger.