Rushwa yamponza rais wa zamani Brazil

BRASILIA-
RAIS zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva (pichani), amehukumiwa kifungo cha
miaka tisa na miezi sita jela kutokana na kesi tano za ulaji rushwa
zinazomkabili.
Kiongozi
huyo wa zamani wa chama cha muungano, alijizolea umaarufu kutoka jamii ya
kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha Brazil.
Lakini sasa,
mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni 1
za malipo ya ghorofa la mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya
ujenzi ya Kibrazil, iitwayo kwa kifupi OAS.
Hukumu hii
inakuja wakati ambapo, Lula ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia
katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani.
Kufuatia
hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa
hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili
wanaomtetea wakiapa kukata rufaa.
Wakati huo
huo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil, inajadili iwapo iiruhusu Mahakama Kuu
kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais Michel Temer.
Temer
alishtakiwa mwezi uliopita, kwa tuhuma za kupokea hongo kutoka kampuni kubwa ya
usindikaji nyama.
Kamati hiyo
inatarajiwa kupiga kura hapo kesho. Iwapo pendekezo hilo litapita, suala hilo
litajadiliwa katika bunge dogo la wawakilishi, ambapo theluthi mbili
itahitajika kupiga kura ili Rais ashitakiwe.
BBC
No comments