Trump aweka video ‘akiipiga’ CNN
WASHINGTON DC- RAIS Donald Trump amechapisha video katika mtandao
wa Twitter, ikimuonesha akimpiga mtu aliye na nembo kichwani ya shirika la
habari la CNN.
Video hiyo
iliyohaririwa (edited) ni ile inayomuonesha Trump wakati akihudhuria michezo ya
mieleka ya WWE mwaka 2007, ambapo 'alimshambulia' mmiliki wa michezo hiyo,
Vince McMahon.
Video hiyo
inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii. CNN
baadaye ilimlaumu Rais kwa kuibua ghasia dhidi ya vyombo vya habari.
Mchambuzi
mmoja katika kituo cha ABC, Ana Navarro, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Trump,
alisema kuwa video hiyo ni uchochezi na huenda ikasababisha mwandishi kuuliwa.
Lakini
mshauri wa masuala ya usalama nchini, Thomas Bosset, ambaye awali alihojiwa na
kituo cha ABC, alisema video hiyo haionekani kuwa tishio.
Mara kwa
mara Rais Trump amekuwa kwenye mzozo na kituo cha CNN anachodai kuwa hutoa ‘taarifa
bandia’
BBC
No comments