China; Manowari ya Marekani kukaribia kisiwa cha Triton ni uchokozi mkubwa

Manowari ya
USS Stethem
BEIJING- CHINA imetaja hatua ya manowari ya Marekani kupita
karibu na kisiwa kinachozozaniwa Kusini mwa bahari ya China, kuwa uchokozi
mbaya wa kisiasa na kijeshi.
Manowari ya
USS Stethem ilipita karibu na kisiwa kinachozozaniwa cha Triton, ambacho ni
moja ya visiwa vinavyodaiwa na China na nchi zingine.
Mara baada
ya manowari hiyo ya Marekani kupita hapo, China ilijibu hatua hiyo haraka kwa
kutuma melivita na ndege kwenda kisiwani humo.
Kisa
hicho kilitokea muda mfupi, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kufafanya. Marekani
mara kwa amara imeionya China dhidi ya hatua yake ya kunyakua visiwa katika
maeneo yanayozozaniwea, lakini China inasema inafanya hivyo kuambatana na haki
zake.
China
inasema kuwa itafanya kila iwezalo kulinda usalama wake. Pia imeilaumu Marekani
kwa kuchochea vurugu eneo hilo, kwa kuwa uhusiano kati ya China na majirani
wake wa Kusini mwa bahari ya China umeimarika.
Kisiwa hicho
kidogo pia kinadaiwa na Vietnam na Taiwan. China imekuwa kwenye mzozo wa
umiliki wa maeneo ya bahari na majirani zake kadhaa miaka ya hivi karibuni.
No comments