Trump adaiwa kukutana kwa siri na Putin
WASHINGTON
DC- IMEBAINIKA kuwa Rais Donald Trump alikutana na mwenzake wa Urusi, Vladmir
Putin katika mkutano wa pili wa siri ambao haukutajwa ulipofanyika katika kikao
cha mkutano wa mataifa ya G20.
Inadaiwa kuwa,
walifanya mazungumzo baada ya mkutano wao wa kwanza, lakini ikulu ya White
House haijatoa maelezo kuhusu kile kilichozungumziwa.
Rais Trump
amekana madai ya kufanyika kwa mkutano huo wa siri na Putin na kusema ni ‘habari
bandia’. Uhusiano wa viongozi hao wawili unachunguzwa, kufuatia madai kwamba
kampeni timu ya Trump ilishirikiana na Urusi.
Wapelelezi
wa Marekani, wanaamini kwamba Urusi ilimsaidia Trump kushinda uchaguzi wa mwaka
jana kitu ambacho Urusi imekana.
Trump
amepinga madai kama hayo. Mkutano huo wa pili, unadaiwa kufanyika wakati wa
chakula cha jioni cha viongozi katika kikao hicho cha G20 mjini Hamburg mapema
mwezi huu
Rais Trump
alikuwa pekee wakati Putin alikuwa na mkalimani wake, huku vyombo vya habari
vya Marekani vikisema mkutano huo ulidumu kwa muda wa saa moja.
Madai ya
kilichozungumzwa yaliwasilishwa kwa maofisa wa Ikulu ya Whitehouse na Trump
mwenyewe, kwa kuwa hakukuwa na wasaidizi wakati wa mkutano huo.
BBC.
No comments