Tembo amuua mwongoza watalii Zimbabwe
HARARE- MWONGOZA
watalii mmoja wa kampuni ya Adventure Zone, Enock Kufandanda, ameuawa na tembo
wakati alipokuwa akiwafuata kwa ajili ya kuwatembeza.
Kwa mujibu
wa taarifa ya kampuni hiyo ya kitalii ya Adventure Zone, Kufandanda aliuliwa jana
jioni na tembo aitwaye Mbaje.
Adventure
Zone ilisema kuwa Kufandada alikuwa mfanyakazi mzuri aliyejitolea hivyo kifo
chake ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo. Mara baada ya tembo huyo kufanya mauaji
hayo, naye aliuawa.
BBC.
No comments