Nigeria watoa picha za Buhari akiwa London
LAGOS- IKULU
ya Nigeria, imetoa picha za Rais Muhammadu Buhari akiwa mjini London, Uingereza
kwa mara ya kwanza tangu andoke nchini karibu siku 80 zilizopita.
Rais Buhari
mwenye umri wa miaka 74, alisafiri kwenda Uingereza kupata matibabu ya ugonjwa
ambao haujawekwa wazi. Jana, Rais Buhari alikutana na magavana wa chama chake
ambapo alionekana mwenye furaha.
Kutokuwepo
kwake kumezua wasi wasi nchini, huku wengi wakidai kuwa huenda amefariki. Wengine
wana hofu kuwa huenda asiwe na uwezo wa kurudi kazini.
Buhari
aliondoka Nigeria mnamo Mei 7, mwaka huu ikiwa ni safari yake ya pili kwenda Uingereza
kupata matibabu. Madaraka yake kwa sasa yanakimiwa na Makamu wa Rais, Yemi
Osinbajo.
No comments