Shambulio la msikitini lajeruhi watu 8 Ufaransa

PARIS- WATU 8 wamejeruhiwa wakati wa ufyataajia risasi
nje ya mskikiti uliopo Kusini mwa nchi.
Waumini
waliokuwa wakiondoka kwenye msikiti wa Al Rahma, walikaribiwa na washukiwa
wawili waliokuwa na bunduki ambao waliwashambulia kwa risasi. Polisi wanasema
kuwa hawachukulii kisa hicho kuwa cha kigaidi.
Watu
wanne walijeruhiwa nje ya msikiti huo, huku wanne wakiwa wa familia moja
akiwemo msichana wa miaka 7. Wawili kati ya watu 8 waliojeruhiwa walilazwa
hospitalini.
Mashuhuda wanasema
kuwa, watu kadhaa wa karibu na msikiti walianza kukimbia wakati walipowaona
washukiwa wawili wakiteremka kwenye magari yao na kuwakaribia wakiwa na bunduki
mikononi.
Kisa cha
Avigno hakichukuliwi kama cha kigaidi, ofisi mkuu wa mshataka ilisema. Kwa sasa
idara ya ujasusi inakifuatilia kisa hicho.
No comments