Header Ads

Mafuriko yaua watu 8 China



https://pbs.twimg.com/media/DDyibGvWAAIldxB.jpg:large
NANNING— WATU nane wamekufa na wengine zaidi ya 250,000 kupoteza mali zao, baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko makubwa ambayo yamesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Kusini mwa nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka za mji wa Guangxi Zhuang, watu tisa wanaripotiwa kupotea huku wengine 34 kujeruhiwa baada ya mafuriko kuvunja zaidi ya nyumba 600 na kuharibu hekta 17,000 za mazao.
Hata hivyo, tayari wananchi zaidi ya 38,000 wamefanikiwa kuhamishwa na kupelekwa katika maeneo salama yenye huduma mbalimbali za kijamii kama vile malazi, huduma za afya, maji na chakula.
Mwishoni mwa wiki, Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (NMC), ilieleza kuwa mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha Jumapili na Jumatatu usiku katika miji ya Guangxi na Hunan.
Xinhua

No comments

Powered by Blogger.