Polisi waua washukiwa wawili wa mauaji ya Kibiti
Jeshi la Polisi limeua watuhumiwa
wawili wa uhalifu maeneo ya ikwiriri katika operesheni ya kusaka wauaji katika
Kanda maalum ya kipolisi Rufiji inayohusisha wilaya za Mkuranga,Kibiti na
Rufiji mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo,Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi,Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya
Jumatano Julai 5 majira ya saa nne usiku katika msitu wa Ngomboroni kata ya
Ikwiriri,Wilaya ya Ikwiriri Kanda maalumu ya Rufiji ambapo askari wa operesheni
maalum wakiwa katika doria za ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na
mauaji yanayoendelea katika Kanda hiyo ya kipolisi.Sabas alisema Askari wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo ambaye alikuwa amekamatwa na baada ya mahojiano alikubali kwenda kuwaonesha Polisi mahali ambapo ni maficho ya wenzake.
Sabas alieleza kuwa, baada ya kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia.
Polisi
kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu
mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa
polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo
idadi yao kufikia wawili.
Majeruhi hao wawili walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata.Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Katika tukio hilo, tumefanikiwa kupata silaha mbili ambazo moja ni ya aina ya SMG na nyingine ni shotgun moja pamoja na risasi tisa za SMG zilizokuwa kwenye Magazine,” alisema Sabas.
Aidha,mkuu huyo wa Operesheni maalum za Jeshi la Polisi Naibu kamishina Sabas ameendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu wengine waliosalia.

Pia,
aliongeza kwamba zawadi nono bado ipo pale pale na itatolewa kwa mtu yeyote
atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika
kanda maalumu ya Rufiji.
Chanzo: ITV
Chanzo: ITV
No comments