Header Ads

Polisi Afrika Kusini kumlinda mkosoaji wa Zuma



Bi Khoza amemtaka Bwana Zuma aondoke madarakani akimtaja kuwa kiongozi wa kuchukiza ambaye amekumbwa na madai ya ufisadi.

CAPE TOWN- MKOSOAJI mashuhuri wa Rais Jacob Zuma, Makhosi Khoza atapewa ulinzi maalum wa polisi baada ya kupokea vitisho vya kuuliwa.
Khoza ambaye ni mbunge kutoka chama tawala cha ANC, analazimika kupewa ulinzi huo baada ya uchunguzi uliofanywa na Polisi pamoja na Bunge kubaini uwepo wa vitisho vya kuuliwa kwa mwanasiasa huyo.
Mara kwa mara, Khosa amekuwa akimtaka Rais Zuma kung’atuka madarakani kutokana na madai ya rushwa na ufisadi ambayo yanamwandama.
Zuma anakana kufanya lolote baya na hakuna madai kuwa amehusishwa na vitisho hivyo.
BBC

No comments

Powered by Blogger.