Msishiriki tendo la ndoa usiku wa kuamkia uchaguzi - Raila
NAIROBI- MGOMBEA
wa urais kupitia muungano wa NASA nchini, Raila Odinga amewataka wafuasi wake
kutoshiriki tendo la ndoa mkesha wa siku ya uchaguzi.
Odinga
amefananisha uchaguzi huo na vita, akisema kuwa kushiriki ngono kabla ya kwenda
vitani ni mkosi mbaya ambao unaweza kusababisha mtu kushindwa.
“Tunaenda
vitani na ni lazima tuhifadhi nguvu zetu kabla ya siku ya vita ambayo ni Agosti
8. Hakuna hata mmoja wetu ambaye anafaa kushiriki ngono kabla ya mkesha wa siku
ya uchaguzi,” Raila aliwaambia wafuasi wake Homa Bay.
Odinga aliwasisitizia
zaidi wanaume, akisema itasababisha wengi wao kutopiga kura. Kwa wanawake,
Raila alisema hawafai kukubali kushiriki tendo hilo na waume zao usiku wa
kuamkia siku ya uchaguzi.
“Kila
mwanamke anafaa kumnyima mumewe haki yake ya tendo la ndoa. Hatua hiyo
itatufanya kuamka mapema alfajiri, ili kupiga kura na kulinda kura na kuilinda
siku nzima hadi pale kura zitahesabiwa na kutangazwa,” alisema kiongozi huyo.
Siyo mara ya
kwanza kwa kiongozi huyo wa chama cha ODM, kukataza tendo la ngono wakati wa
uchaguzi.
Wakati wa
uzinduzi rasmi wa kampeni za muungano wa NASA mjini Kakamega, mnamo Juni 3
mwaka huu, Odinga aliwaambia wafuasi wake kusubiri hadi pale matokeo
yatakapotangazwa ili kuweza kufurahia tendo hilo la ndoa.
“Nawaomba
wanawake, muwaambie waume zenu wasubiri hadi baada ya uchaguzi ili kuweza
kushiriki tendo hilo ili kusherehekea ushindi wetu,” alisema Raila.
BBC
No comments