Mkuu wa mawasiliano ikulu ya Marekani ajiuzulu
WASHINGTON
DC- Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Ikulu ya White House, Sean Spicer
amejizulu.
Taarifa zinaeleza
kuwa, Spicer amejiuzulu kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika kitengo
hicho.
Kwa mujibu
wa gazeti la New York Times, Spicer ameng'atuka kutoka kwenye wadhifa wake, kwa
sababu hajaridhishwa na hatua ya Rais Donald Trump kumteua Anthony Scaramucci kuwa
Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano.
Mshirika
mkuu katika soko la Wall Street, Scaramucci ameteuliwa kuhudumu katika wadhifa
huo ambao Spicer alifanikiwa kutekeleza sehemu ya majukumu yake.
Vikao vya
Spicer na wanahabari vilikuwa maarufu, lakini hajahutubia wanahabari wiki za
karibuni.
Mabadiliko
kwenye kitengo hicho, yametokea wakati ambapo ikulu ya White House inakabiliwa
na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa urais wa mwaka jana kumsaidia
Trump kushinda.
Aidha, kuna
tuhuma kwamba maofisa wa kampeni wa Trump huenda walishirikiana na maofisa wa Urusi.
Gazeti hilo linasema kuwa Spicer, 45, alipinga vikali kuteuliwa kwa Scaramucci.
BBC.
No comments